VIJANA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU WAJITENGA NA MAANDAMANO YA 7/7
VIJANA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU WAJITENGA NA MAANDAMANO YA 7/7
Na mwandishi wetu Wakati baadhi ya wanaharakati na watumiaji wa mitandao ya Kijamii wakihamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii kuelekea Julai 7, 2026, vijana wanaoishi katika mazingira magumu ambao walijikuta katikati ya vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 wameeleza namna walivyobeba mzigo mkubwa wa madhara, wakisema hawatamani kuona hali kama hiyo ikijirudia. Vijana hao wanasema kipindi hicho kilisababisha kukosekana kwa amani, chakula, sehemu za kulala na shughuli za kujipatia kipato, huku baadhi ya wenzao wakijeruhiwa, kupata ulemavu wa kudumu na wengine kupoteza maisha. Mmoja wao, Juma Maftah, mkazi wa Ilala Dar Es Salaam amesema siku za vurugu zilikuwa ngumu zaidi kwa watu wanaoishi mitaani kuliko kundi lolote lingine. “Tarehe 29, 2025 wakati ule kilichotokea ilikuwa changamoto sana kwangu, amani hakuna, kula ilikuwa tabu, sehemu za kulala pia kwa sisi tunaolala nje ilikuwa changamoto sana, wengine walivunjika miguu na ndugu zetu wengine walikufa. Ilifika hatua mpaka tukawa …