VIJANA WAHIMIZWA KUPATA ELIMU YA FEDHA WAKATI COOP BANK IKIPANUA WIGO WA HUDUMA ZAKE

VIJANA WAHIMIZWA KUPATA ELIMU YA FEDHA WAKATI COOP BANK IKIPANUA WIGO WA HUDUMA ZAKE
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv WAZIRI katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, amewataka vijana nchini kuzingatia elimu ya fedha akisema ni nyenzo muhimu ya kuwawezesha kiuchumi na kuwapa uwezo wa kushiriki kikamilifu katika agenda ya maendeleo ya taifa. Nanauka ametoa wito huo leo Mei 5, 2026 wakati akizindua tawi jipya la Benki ya Ushirika (Coop Bank) jijini Dar es Salaam, ambalo ni tawi la sita la benki hiyo tangu kuanzishwa kwake. Uzinduzi huo umeambatana na kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya Coop Bank na Wizara ya Maendeleo ya Vijana yenye lengo la kuwajengea vijana maarifa ya kifedha na kuongeza ushiriki wao katika miradi mbalimbali ya maendeleo. Akizungumza katika hafla hiyo, Nanauka amesema Coop Bank ni daraja muhimu linalowaunganisha vijana na fursa za kiuchumi pamoja na miradi ya maendeleo. "Elimu ya fedha ni muhimu kwa vijana ikiwa wanataka kuwa huru kiuchumi na kuchangia kwa maana katika maendeleo ya taifa," amesema. Ameong…