Vijana Wahamasishwa Kuwekeza Kwenye Ufagaji Wa Kuku Na Kutumia Chakula Bora Kwa Mifugo

Vijana Wahamasishwa Kuwekeza Kwenye Ufagaji Wa Kuku Na Kutumia Chakula Bora Kwa Mifugo
Na Mwandishi Wetu WAFUGAJI wa kuku nchini wamehimizwa kutumia chakula bora cha mifugo ili kuongeza uzalishaji, kuboresha afya ya kuku na kuongeza faida ya biashara zao, huku vijana wakitakiwa kuchangamkia fursa za ufugaji wa kuku kama njia ya kujiajiri na kujikwamua kiuchumi. Wito huo unakuja sambamba na upanuzi wa huduma za kampuni ya Ekama Animal Feeds ambayo imefungua rasmi tawi jipya la Gongolamboto, Dar es Salaam, litakaloanza kutoa huduma kuanzia Julai 1, 2026 kwa lengo la kuwasogezea wafugaji bidhaa na huduma za kitaalamu. Kupitia tawi hilo jipya lililopo eneo la Mombasa-Gongolamboto, wafugaji watapata huduma za ushauri wa kitaalamu kutoka kwa madaktari wa mifugo bila malipo pamoja na huduma za usafiri bure, hatua inayolenga kupunguza gharama na kuwawezesha kupata huduma kwa urahisi. Akizungumza na Wadau wa sekta ya mifugo,Meneja mauzo kutoka kampuni ya Ekama Animal Feeds Irene Temba amesema matumizi ya chakula bora ni msingi wa mafanikio katika ufugaji wa kuku kwani huchangia kuku…