VIJANA NCHINI KUNUFAIKA NA MPANGO MPYA WA SERIKALI WA UTAMBUZI NA UWEZESHAJI
VIJANA NCHINI KUNUFAIKA NA MPANGO MPYA WA SERIKALI WA UTAMBUZI NA UWEZESHAJI
Na Janeth Raphael MichuziTv - Bungeni Dodoma Serikali imesisitiza dhamira yake ya kuwatambua na kuwawezesha vijana nchini kwa kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa takwimu na kuongeza fursa za kiuchumi na kijamii kwa kundi hilo muhimu la maendeleo ya taifa. Akijibu swali bungeni leo lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Latifa Khamis Juwakali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, amesema Serikali inalitambua kundi la vijana kama nguzo muhimu ya maendeleo ya nchi. Waziri Nanauka amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha vijana wanatambuliwa rasmi kupitia zoezi la Utambuzi wa Vijana (Youth Mapping) linaloratibiwa na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana. Ameeleza kuwa zoezi hilo litasaidia kupata takwimu sahihi kuhusu idadi ya vijana, mahitaji yao halisi, pamoja na changamoto zinazowakabili, hatua itakayosaidia kupanga na kutekeleza afua zenye tija zaidi katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Aidha, Serikali imeendelea kutekeleza programu mbalimbali…