VIJANA NA WASOMI MKOANI MWANZA WAHIMIZWA UZALENDO NA UJASIRIAMALI KATIKA KONGAMANO
VIJANA NA WASOMI MKOANI MWANZA WAHIMIZWA UZALENDO NA UJASIRIAMALI KATIKA KONGAMANO
Na Mwandishi Wetu Katika jitihada za kuimarisha chachu ya maendeleo, Kongamano la Wasomi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Seneti Mkoa wa Mwanza, limefanyika leo, Juni 07, 2026, katika Chuo cha Uvuvi Nyegezi, likilenga kuwajengea vijana uwezo katika nyanja za uongozi, uchumi, afya, na itikadi ya chama. Akizungumza katika kongamano hilo, Mgeni Rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Vyuo na Vyuo Vikuu Seneti Mkoa wa Mwanza, Kenneth Geremia, amewasisitiza vijana kuonesha mapenzi ya dhati kwa Chama Cha Mapinduzi. Kiongozi huyo mwenye maono mapana, amewataka wanachama kudumisha mshikamano na ushirikiano imara baina ya matawi yote ndani ya mkoa wa Mwanza ili kujenga chama chenye nguvu zaidi. Katibu wa Vijana UVCCM Kata ya Luchelele, Omary Msuya, aliyekuwa mratibu wa hafla hiyo (MC), ametoa wito mzito kwa kila kijana kufanya uwajibikaji na uzalendo kuwa kipaumbele chao cha kwanza katika ujenzi wa taifa, akisisitiza kuwa vijana ndio uti wa mgongo wa maendeleo. Kwa upande…