VIJANA 240 KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA UFUNDI KUPITIA MRADI WA DUMISHA AMANI
VIJANA 240 KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA UFUNDI KUPITIA MRADI WA DUMISHA AMANI Vijana 240 katika wilaya za Mtawara, Lindi, Songea na Kigoma wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya ufundi stadi kupitia mradi wa “Dumisha Amani” unaofadhiliwa na mashirika ya kimataifa ya UNPDF, UNDP-Tanzania na kampuni ya CPP. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, tarehe 29 Juni 2026, katika chuo cha VETA Mtwara, Afisa Mkuza Mitaala Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Alphoncina James Mshana amesema mafunzo kwa vijana hao yatatolewa kwenye vyuo vya VETA katika wilaya husika na yatafanyika kwa muda wa wiki mbili yakihusisha stadi za ufundi Umeme, Maabara, Upishi na Upambaji. Amesema, katika wilaya ya Mtwara pekee, vijana 60 wanatarajiwa kunufaika na mafunzo hayo. Ameongeza, sambamba na stadi za ufundi vijana hao pia watafundishwa Ujasiriamali na Stadi za Maisha, ili kuwajengea uwezo wa kutumia ujuzi wao kuanzisha biashara ndogo ndogo zinazohusiana na sekta za uchumi wa buluu. Mshana amewashukuru wafadhili hao akieleza kuwa uhusiano mkubwa kati ya amani …