VIJANA 10 WATINGA FAINALI SHINDANO LA VIJANA UCHUMI CHALLENGE 2026

VIJANA 10 WATINGA FAINALI SHINDANO LA VIJANA UCHUMI CHALLENGE 2026
Na Victor Masangu, Pwani Vijana wapatao kumi kutoka baadhi ya mikoa mbali mbali wamefanikiwa kutinga katika kinyang'anyiro cha shindano la Vijana uchumi Challenge kwa mwaka wa 2026 ambalo kilele chake kinatarajiwa kufanyika Julai 6 mwaka huu katika ukumbi Mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), jijini Dar es Salaam. Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Jenifa Omolo ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa halfa ya kufunga kambi rasmi ya vijana wapatao 100 ambao walikuwa wameweka kambi ya siku nne katika shule yaa uongozi wa Mwalimu Julias Nyerere iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani. Katibu Oomolo amesema kwamba kambi hiyo ilikuwa na vijana wapatao 100 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania bara na visiwani ambapo wameweza kufanyiwa usahili na kufanyiwa mchujo kutoka kwa majaji mahiri wapatao saba ambaao waliweza kuzingatia vigezo mbali mbali katika kufanya maamuzi na kuangalia mawazo ambayo yaliwasilishwa na vijana hao. "…