Veterani UVCCM kuenzi mchango wa Mzee Mtulia

Veterani UVCCM kuenzi mchango wa Mzee Mtulia
NA MWANDISHI WETU VETERANI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wamesema wataendelea kuenzi mchango mkubwa wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, marehemu Mohammed Mtulia. Ahadi hiyo ilitolewa na Veterani Sadick Chamumi, kwa niaba ya Katibu wa Maveterani hao, Mkoa wa Dar es Salaam, walipofika nyumbani kwa marehemu Mzee Mtulia, Mtaa wa Muheza, wilayani Temeke, kuwasilisha rambirambi zao. "Mzee Mtulia ameacha wasifu mkubwa, hivyo inabidi tujifunze kutoka kwake. Kwa niaba ya Mavetarani wa UVCCM, tunaipa pole familia na tutaendelea kushirikiana nayo,”almesema Chamumi. Mzee Mtulia alifariki dunia Mei 5, mwaka huu, nyumbani kwake Mtaa wa Mkuranga B, wilayani Temeke. Naye, Katibu Msaidizi wa Veterani wa UVCCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Justy Mboke, ameeleza Mzee Mtulia enzi za uhai wake alifanya mambo makubwa, hususan kuimarisha mabaraza ya wazee kuanzia ngazi za tawi, kata, wilaya hadi mkoa. “Mabaraza hayo mpaka hivi sasa yanafanya kazi. S…