VETA YAZALISHA BIDHAA 825 KUPITIA KAMPUNI YA TANZU YA UJUZI, ZASAMBAZWA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR
VETA YAZALISHA BIDHAA 825 KUPITIA KAMPUNI YA TANZU YA UJUZI, ZASAMBAZWA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR
Na Wellu Mtaki, Dodoma MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kupitia Kampuni Tanzu ya Ujuzi ya VETA, imefanikiwa kuzalisha bidhaa 825 ambazo tayari zimesambazwa katika taasisi mbalimbali za serikali pamoja na hoteli zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha matumizi ya ujuzi wa ufundi katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora na thamani ya kiuchumi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Meneja wa Kampuni Tanzu ya Ujuzi ya VETA, Mhandisi Marco Kapinga, amesema kampuni hiyo imeendelea kutumia maarifa na ujuzi unaopatikana kupitia mafunzo ya VETA kuzalisha bidhaa mbalimbali zinazokidhi mahitaji ya taasisi za umma, sekta binafsi na makundi tofauti ya jamii. Amesema mafanikio hayo yanaonesha namna mafunzo ya ufundi stadi yanavyoweza kuchangia moja kwa moja katika maendeleo ya uchumi wa nchi kupitia uzalishaji wa bidhaa na huduma zenye viwango vinavyokubalika sokoni. “Lengo letu si tu kuza…