UTALII WA NDANI WATAKIWA KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA KUKUZA SEKTA YA UTALII TANZANIA

Meneja wa Moyo Tented Camps inayomilikiwa na kampuni ya Conservation Caravan Safaris, Mary Loishooki akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha …………….. Na Happy Lazaro, Arusha Wakati juhudi za kuitangaza Tanzania kama moja ya destinisheni bora za utalii duniani zikiendelea kuongezeka, Watanzania wametakiwa kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kushiriki kikamilifu katika kuvitangaza kwa manufaa ya taifa na uchumi wake. Wito huo umetolewa jijini Arusha na Meneja wa Moyo Tented Camps inayomilikiwa na kampuni ya Conservation Caravan Safaris, Mary Loishooki, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchango wa sekta binafsi katika kukuza utalii pamoja na huduma zinazotolewa na kampuni hiyo kwa wageni wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Loishooki amesema kuwa mara nyingi Watanzania wamekuwa wakivichukulia kawaida vivutio vilivyopo nchini huku wageni kutoka mataifa mbalimbali wakisafiri maelfu ya kilomita kuvitembelea, jambo ambalo linaon…