UKEREWE YATOA SH. MILIONI 586.5 KWA VIKUNDI 57, DC NGUBIAGAI ASISITIZA MAPINDUZI YA KIUCHUMI

UKEREWE YATOA SH. MILIONI 586.5 KWA VIKUNDI 57, DC NGUBIAGAI ASISITIZA MAPINDUZI YA KIUCHUMI
Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cde. Christopher Ngubiagai Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani inaendelea kuzaa matunda, huku Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ikitekeleza kwa vitendo maelekezo hayo kwa kutoa mikopo yenye thamani ya Shilingi milioni 586.5 kwa vikundi 57 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Hatua hiyo inaakisi dhamira ya Serikali ya kuhakikisha makundi maalum yanapata fursa za kiuchumi, kujiongezea kipato, kujiajiri na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa taifa unaojumuisha wananchi wote. Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo hiyo iliyofanyika Juni 10, 2026 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Bukongo, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Christopher Ngubiagai, amesema utekelezaji wa mikopo hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Rais Samia za kuwainua wananchi kiuchumi na kuharakisha maendeleo …