UJENZI WA DARAJA KATA YA MKULULU WAONDOA KERO YA USAFIRI WAKUZA UCHUMI WILAYANI MASASI

UJENZI WA DARAJA KATA YA MKULULU WAONDOA KERO YA USAFIRI WAKUZA UCHUMI WILAYANI MASASI
Masasi, Mtwara ‎Wananchi wa kata ya Mkululu na maneno jirani wilayani Masasi mkoani Mtwara wameanza kunufaika na huduma bora za usafiri na usafirishaji kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa daraja katika barabara ya Chingutwa–Songambele. ‎Ujenzi huo uliotekelezwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia mradi wa RISE programu ya uondoaji vikwazo vya barabara (Botleneck) umekuwa na manufaa makubwa hasa urahisi wa usafirishaji wa mazao ya wakulima. ‎Meneja wa TARURA wilaya ya Masasi, Mhandisi John Kimario amesema changamoto kubwa iliyokuwa inawakabili wananchi ni usafirishaji wa mazao ya mashambani kwa sababu katika wilaya hiyo wananchi wanategemea kilimo cha korosho, ufuta na mbaazi.  ‎”Mfumo wa uuzaji wa mazao ni kupitia maghala kwa maana yanapitishwa ghalani halafu yanasafirishwa kwenda maeneo mengine. Kabla ya ujenzi wa daraja hili usafirishaji wa mazao haya kutoka mashambani kwenda kwenye maghala ilikuwa ni changamoto kubwa”, amesema Mhandisi Kimario. ‎Amesema baada ya u…