UCSAF Yajivunia Kupeleka Mawasiliano Vijijini, Zaidi ya Minara 2,000 Yajengwa Nchini.
UCSAF Yajivunia Kupeleka Mawasiliano Vijijini, Zaidi ya Minara 2,000 Yajengwa Nchini.
Na Belinda Joseph- Dodoma. Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeendelea kuwa nguzo muhimu katika kusogeza huduma za mawasiliano karibu na wananchi, hususan waishio maeneo ya vijijini yasiyo na mvuto wa kibiashara kwa kampuni za mawasiliano. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Mhandisi Wilfred Charles kutoka UCSAF Juni 21, 2026, amesema ushiriki wao katika maadhimisho hayo unalenga kuielimisha jamii kuhusu majukumu na miradi mbalimbali inayotekelezwa na mfuko huo katika kuboresha huduma za mawasiliano nchini. Amesema UCSAF kwa kushirikiana na Serikali imekuwa ikitoa ruzuku kwa watoa huduma za mawasiliano ili kuhakikisha huduma hizo zinafika katika maeneo ya vijijini ambayo kwa kawaida hayavutii uwekezaji wa kibiashara. Ameeleza kuwa Mbali na ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano, UCSAF pia inatekeleza mradi wa utoaji wa huduma za WiFi katika maeneo ya wazi, pamoja na kupanua usikivu wa Redio ya Taifa na redio za kijamii katika maeneo mbalimbali nchini, hatua …