TVLA YAWATAKA WAFUGAJI KUONGEZA MWITIKIO WA CHANJO ZA MIFUGO

TVLA YAWATAKA WAFUGAJI KUONGEZA MWITIKIO WA CHANJO ZA MIFUGO
Farida Mangube Morogoro  Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi, amewataka wafugaji kuongeza mwitikio wa kuchanja mifugo ili kudhibiti magonjwa, kuongeza uzalishaji na kulinda afya ya binadamu.  Akizungumza Juni 18, 2026 mjini Morogoro katika kikao kati ya TVLA na timu ya Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), amesema wafugaji wadogo bado wanaitikia kwa kiwango cha chini kampeni za chanjo licha ya upatikanaji wa chanjo zinazozalishwa na TVLA, huku akisisitiza umuhimu wa elimu kwa wafugaji ili kupunguza magonjwa ya mifugo. Dkt. Bitanyi amesema mradi wa C-SDTP unapaswa kusaidia utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa chanjo na kushirikiana katika kudhibiti ugonjwa wa tupa mimba (Brucellosis) pamoja na magonjwa mengine yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.  Pia amewahimiza wananchi kutumia maziwa salama kwa kuyachemsha kabla ya matumizi, akibainisha kuwa TVLA inaendelea kuzalisha chanjo, kufanya taf…