TUZO ZA MAKAMPUNI BORA 100 ZA CHAPA AFRIKA ZATAJWA KUCHOCHEA MAENDELEO SEKTA BINAFSI.

TUZO ZA MAKAMPUNI BORA 100 ZA CHAPA AFRIKA ZATAJWA KUCHOCHEA MAENDELEO SEKTA BINAFSI.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, amesema wazalishaji, wafanyabiashara na watoa huduma nchini ni nguzo muhimu katika maendeleo ya uchumi kutokana na mchango wao katika uzalishaji, biashara na utoaji wa huduma mbalimbali na jitihada zao zinapaswa kutambuliwa ili kuhamasisha utendaji bora na kuongeza ushindani wenye tija. Londo amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa utambuzi wa kampuni bora 100 za chapa za Afrika zinazotengeneza bidhaa zilizoko barani humo, jijini Dar es Salaam. Amesema serikali inatambua mchango wa Wafanyabiashara na wazalishaji, na ni njia mojawapo ya kuwapa hamasa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi katika shughuli zao za kiuchumi. "Mwaka huu ni wa kihistoria kutokana na kupitishwa kwa bajeti itakayoweka msingi wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050, ambapo sekta binafsi inatarajiwa kuwa mhimili mkubwa wa ukuaji wa uchumi,hivyo Serikali inaitambua sekta binafsi kama mdau muhimu katika kufanikisha maendeleo ya Taifa",a…