TRA YAKUSANYA TRILIONI 32.3 BAADA YA MIAKA 30 YA MAGEUZI YA KODI
TRA YAKUSANYA TRILIONI 32.3 BAADA YA MIAKA 30 YA MAGEUZI YA KODI John Bukuku, Dar es Salaam Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa katika kipindi cha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake imepata mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, ambapo makusanyo yameongezeka kutoka shilingi bilioni 538 kwa mwaka hadi kufikia shilingi trilioni 32.3 katika mwaka wa fedha 2025/2026. Kauli hiyo amesema Kamishna Mkuu wa TRA, CPA Yusuf Mwenda, wakati akizungumza katika Kongamano la Pili la Kodi la TRA (TRA Tax Symposium 2026) linalofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Juni 19, 2026, likiambatana na maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996. Amesema TRA imeendelea kufanya mageuzi makubwa ya kiutendaji kwa lengo la kuboresha huduma kwa walipa kodi, kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kujenga mfumo unaochochea ulipaji kodi kwa hiari. CPA Mwenda amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na ushirikiano mkubwa kati ya TRA, walipa kodi, wafanyabiashara na wadau mbalimbali ambao wamekuwa sehemu muhimu…