TRA YAKABIDHI VIFAA TIBA VYA SH. MILIONI 162 HOSPITALI YA RUFAA YA MWANANYAMALA

TRA YAKABIDHI VIFAA TIBA VYA SH. MILIONI 162 HOSPITALI YA RUFAA YA MWANANYAMALA
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 162 katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya TRA na utoaji wa Tuzo za Rais kwa Mlipakodi Bora zinazotarajiwa kutolewa Julai Mosi mwaka huu Mlimani City Jijini Dar es Salaam.  Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Hospitalini hapo Juni 28, 2026 Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema wameamua kurudisha kwa jamii mchango wa kodi ambazo wananchi wamechangia ili zisaidie kutoa huduma. Amepongeza uwekezaji wa majengo uliopo Hospitalini hapo na kueleza kuwa ni matunda ya kodi ambayo yamewezesha maboresho hayo huku akisisitiza kuwa msaada wa vifaa hivyo ni hatua ya TRA kurejesha kwa jamii kutokana na kodi  zinazokusanywa na baadae kurudi kwa watanzania kwa njia mbalimbali ikiwepo kuimarisha huduma za afya. "Tumekuja leo kwa sababu  mwezi wa saba TRA itatimiza miaka ya  30 ya kufanya kazi tuliyotumwa na watanzania n…