TRA IRINGA YATANGAZA WIKI YA SHUKRANI KWA MLIPAKODI NA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA TRA

TRA IRINGA YATANGAZA WIKI YA SHUKRANI KWA MLIPAKODI NA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA TRA
NA DENIS MLOWE - IRINGA MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Iringa imezindua rasmi ratiba ya matukio yatakayofanyika kuanzia Juni 22 hadi Juni 27, 2026, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mlipakodi kwa mwaka wa kodi 2024/2025 pamoja na kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari,Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa, Maigloria Saria, alisema maadhimisho hayo yanalenga kutoa shukrani kwa walipakodi, kuimarisha elimu ya kodi na kuendelea kujenga ushirikiano kati ya TRA na wadau mbalimbali wa maendeleo. Alisema shughuli hizo zitaanza Juni 22 kwa zoezi la upandaji miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamin Sitta. Bi Saria alisema kuwa Juni 24 na 26 TRA itafanya ziara katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo kwa lengo la kuwashukuru walipakodi kwa mchango wao katika maendeleo ya taifa kupitia ulipaji wa kodi kwa hiari. Aidha, Juni 23 kutafanyika jukwaa la wadau litak…