TCPM YAANZA RASMI USAMBAZAJI WA NGUZO ZA ZEGE KWA WATEJA
TCPM YAANZA RASMI USAMBAZAJI WA NGUZO ZA ZEGE KWA WATEJA *Ni zile zinazozalishwa katika Kiwanda cha Nguzo za Zege Mkoani Tabora *Lengo ni kuboresha miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme kwa wateja Kampuni tanzu ya TANESCO ya kuzalisha nguzo za zege (TCPM) imeanza rasmi kusambaza nguzo za zege zinazozalishwa katika Kiwanda cha Nguzo za Zege kilichopo Mkoa wa Tabora, kwa lengo la kuimarisha na kuboresha miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini. Akizungumza Juni 4, 2026, wakati wa zoezi la upakiaji wa nguzo hizo kwa ajili ya kusambazwa katika maeneo mbalimbali nchini, hususani mkoa wa Tabora na mikoa jirani, Kaimu Meneja Mkuu wa TCPM, Mha. Khadija Abdallahmed, ameishukuru Serikali kupitia TANESCO kwa kuwezesha uanzishwaji wa kiwanda hicho, ambacho kinalenga kuimarisha miundombinu ya usambazaji wa umeme kwa wateja. “Tunaishukuru sana Serikali kupitia TANESCO kwa kuwezesha kiwanda hiki. Leo tunashuhudia mafanikio makubwa baada ya kuanza kusambaza nguzo zilizozalishwa katika kiwanda chetu cha Tabora. Nguzo hizi sasa zina…