TCAA Yatumia Wiki ya Utumishi wa Umma Kuelimisha Wananchi

TCAA Yatumia Wiki ya Utumishi wa Umma Kuelimisha Wananchi
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeungana na Taasisi mbalimbali za umma kushiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma kuanzia, Juni 16, 2026. Katika maonesho hayo, TCAA inatoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yake ya msingi, yakiwemo udhibiti wa shughuli zote za usafiri wa anga nchini. Hii inajumuisha pia usimamizi wa matumizi ya droni, ambalo ni eneo linalokua kwa kasi na kuhitaji ufuatiliaji wa karibu siyo tu kwa ajili ya usalama wa anga, bali pia kulinda faragha ya watu na kuepusha matumizi ya vifaa hivyo katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria, kama vile maeneo ya kijeshi, taasisi za serikali, na miundombinu nyeti. Huduma nyingine zinazotolewa na TCAA ni pamoja na utoaji wa huduma za uongozaji ndege kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa safari za anga ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Mamlaka hiyo inatumia fursa hiyo kuwahamasisha vijana na wadau wa sekta ya usafiri wa anga kuch…