TAWIRI YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WADAU MAONESHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
TAWIRI YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WADAU MAONESHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
📍 Chinangali Park, Dodoma TAWIRI imeendelea kutoa elimu kwa wadau wakiwepo wananchi ambapo wakulima wamepata elimu ya umuhimu wa wadudu katika uhifadhi endelevu wa wanyamapori sambamba na mchango wa wadudu katika kilimo ikiwa ni pamoja na uchavushaji. Vilevile wananchi wamepata uelewa juu ya juhudi zinazofanywa na TAWIRI chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii za kuwahifadhi wanyamapori kwa kutumia taarifa sahihi za kisayansi. “tunashukuru kwa elimu nzuri, kabla ya elimu hii nilijua wanyamapori wanakaa porini wanajihudumia lakini leo nimepata uelewa wanyamapori wanatibiwa, wanahesabiwa, wanafuatiliwa mienendo yao kwa kutumia teknolojia” amesema Enderesa Salla miongoni mwa wananchi waliotembelea banda la TAWIRI TAWIRI tunawakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kuja kupata elimu ya sayansi ya wanyamapori kwa ustawi wa uhifadhi na kukuza Utalii.