TANZANIA,JICA KUPANUA USHIRIKIANO KWENYE UTAFITI WA MADINI MUHIMU NA KIMKAKATI

TANZANIA,JICA KUPANUA USHIRIKIANO KWENYE UTAFITI WA MADINI MUHIMU NA KIMKAKATI
-Zaidi ya Wataalamu 30 Wanufaika na mafunzo kupitia Mradi wa  Kizuna 📍 Dodoma Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA) zimekubaliana kupanua wigo wa ushirikiano kwa kubainisha maeneo ya kipaumbele yatakayofadhiliwa kupitia JICA kwa msaada wa Serikali ya Japan ikiwemo utafiti wa madini muhimu na mkakati. Hayo yamebainishwa Juni 25, 2026 jijini Dodoma katika kikao kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika maendeleo ya Sekta ya Madini nchini. Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amesema ushirikiano na taasisi hiyo ni wa muda mrefu ambao kupitia JICA zaidi ya wataalamu 30 wa Sekta ya Madini wamepatiwa mafunzo nchini Japan yaliyowajengea uwezo na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara na taasisi zake na kueleza kwamba, ushirikiano huo utaendelea kuimarishwa kwa manufaa ya Tanzania na Japan. Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa JICA nchini Tanzania, Dkt. Katsuyika Kuge, am…