TANZANIA YAALIKWA KUWA MWENYEJI MAONESHO YA UFUGAJI NYUKI AFRIKA 2028

TANZANIA YAALIKWA KUWA MWENYEJI MAONESHO YA UFUGAJI NYUKI AFRIKA 2028
Na Mwandishi Wetu. TAASISI ya Maonesho ya Ufugaji wa Nyuki barani Afrika ya Africa Bee Expo, imeialika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Tano ya Ufugaji wa Nyuki Afrika yatakayofanyika mwaka 2028 na kujumuisha wafugaji wa nyuki kutoka nchi 50. Mwaliko huo umetolewa Juni 4, 2026 na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Bw. Fatah Ben Chouia wa Algeria, alipokutana na kuzungumza na Balozi wa Tanzania nchini Algeria Mobhare Matinyi, katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers. Pamoja na mwaliko huo, Bw. Chouia aliwasilisha pia mwaliko wa Tanzania kuwa mgeni rasmi katika Maonesho ya Nne ya Ufugaji wa Nyuki Afrika yatakayofanyika jijini Algiers, Algeria, tarehe 3-6 Septemba, 2026, na kuziomba taasisi za serikali na watu binafsi wa Tanzania kushiriki. Balozi Matinyi aliishukuru taasisi hiyo kwa kuipa Tanzania heshima ya ugeni rasmi mwaka 2026 na uenyeji mwaka 2028 na kuahidi kwamba Serikali itaifanyia kazi mialiko hiyo kwa manufaa ya sekta hiyo ambayo hutoa fursa ya ajir…