TANZANIA NA VIETNAM KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KATIKA ELIMU, BIASHARA NA MAENDELEO
TANZANIA NA VIETNAM KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KATIKA ELIMU, BIASHARA NA MAENDELEO Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia Bi .Felista Rugambwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya kisoshalisti ya Vietnam Nchini Tanzania Bi Vu Thanh Huyen ,Juni 19 2026 Jijini Dodoma. Katika mazungumzo hayo, Bi Felista amesisitiza dhamira ya Tanzania kuendeleza na kuimarisha ushirikiano na Vietnam hususani katika sekta ya elimu ya juu. Amesema Tanzania inathamini mchango wa ushirikiano wa kimataifa katika kukuza rasilimali watu, utafiti na ubunifu, na kwamba hatua ya kuunganisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vikuu vya Vietnam itakuwa chachu muhimu ya maendeleo ya elimu na teknolojia kati ya mataifa hayo mawili. Kwa upande wake, Balozi Vu Thanh Huyen ameishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuwezesha upatikanaji wa kiwanja katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba, akieleza kuwa hatua hiyo ni ishara muhimu ya kuimarika kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam. Aidha, Balozi Huyen ameonesha utayari wa Vietnam wa kuend…