TANZANIA NA UJERUMANI ZAIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA MAJI
TANZANIA NA UJERUMANI ZAIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA MAJI Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, amefanya mazungumzo na Kaimu Mkuu wa Idara ya Miradi ya Maendeleo katika Ubalozi wa Ujerumani nchini. Bi. Marlene Landes, jijini Dar es Salaam. Lengo la mazungumzo hayo ni kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Shirikisho la Ujerumani katika kuendeleza Sekta ya Maji. Katibu Mkuu, Mhandisi Mwajuma Waziri amesisitiza kuwa ushirikiano huo ujikite zaidi katika maeneo ya kimkakati ili kuongeza tija katika sekta. Akitaja umuhimu wa kujenga uwezo wa wataalamu ili waendane na mabadiliko ya teknolojia, kupunguza upotevu wa maji na kuimarisha matumizi ya mifumo ya kisasa ya SCADA katika uendeshaji na ufuatiliaji wa miundombinu. Aidha, ameongeza kuwa kuna haja ya kuendeleza matumizi ya Green Bonds kama chanzo mbadala cha fedha za uwekezaji, pamoja na kuhimiza matumizi ya vifaa vyenye ufanisi mkubwa wa nishati ya jua. Mhandisi Mwajuma amebainisha kuwa Sekta ya Maji bado inahitaji v…