TANZANIA NA GIZ ZASAINI MAKUBALIANO YA KUIMARISHA USHIRIKISHWAJI WA WANAWAKE KATIKA TEKNOLOJIA ZA KIDIJITALI.
TANZANIA NA GIZ ZASAINI MAKUBALIANO YA KUIMARISHA USHIRIKISHWAJI WA WANAWAKE KATIKA TEKNOLOJIA ZA KIDIJITALI.
Na Mwandishi Wetu, WMJJWM Dar Es Salaam Serikali ya Tanzania na Ujerumani zimesaini Makubaliano ya Utekelezaji wa Mradi wa Kituo cha Mabadiliko ya Kidijitali Tanzania (Digital Transformation Centre – DTC Tanzania), utakayochochea ushiriki wa wanawake na wasichana katika uchumi wa kidijitali kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa. Akizungumza katika hafla ya utiaji saini baina ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) iliyofanyika jijini Dar es Salaam Juni 11, 2026, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Bw. Badru Alburnoor amesema makubaliano hayo yanafungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya nchi ya Tanzania na Ujerumani katika kuhakikisha wanawake na wasichana wanapata fursa sawa za kushiriki na kunufaika na maendeleo ya teknolojia za kidijitali. Amesema mradi huo unaendana kikamilifu na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Sera ya Tai…