TANZANIA GENERATION CARE YATOA MSAADA WA SARUJI, MABATI NA MATOFALI KWA MZEE LUPITA
TANZANIA GENERATION CARE YATOA MSAADA WA SARUJI, MABATI NA MATOFALI KWA MZEE LUPITA Taasisi ya Tanzania Generation Care imetoa msaada wa mifuko ya saruji, mabati pamoja na matofali kwa ajili ya kumsaidia mlemavu wa macho, Mzee Paulo Lupita, mkazi wa Tabata Mawezi, Dar es Salaam, ambaye nyumba yake imebomoka na hivyo kulazimika kulala nje. Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi msaada huo kwa Mzee Lupita, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Generation Care, Bi. Fauzia Mbwana, amesema taasisi hiyo imeguswa kumsaidia kutokana na hali yake ya uhitaji. Amesema Mzee Lupita pamoja na mke wake ni watu wenye ulemavu na wanahitaji msaada ili kuboresha maisha yao, hasa baada ya kulazimika kuishi nje kufuatia kubomoka kwa nyumba yao. Bi. Mbwana amesema wanaamini msaada huo utasaidia kutatua changamoto inayowakabili kwa kuwezesha ujenzi wa sehemu ya nyumba ambayo ukuta wake ulianguka, hali iliyowalazimu kuishi bila makazi salama. Aidha, amesema kuwa Taasisi ya Tanzania Generation Care imelenga kuboresha maisha ya jamii kwa kutoa elimu ya malezi kwa watoto pamoja na kusai…