TANESCO YAZINDUA MPANGO WA MIKOPO YA MAJIKO YA UMEME NA VITUO VYA KUCHAJI MAGARI YA UMEME
TANESCO YAZINDUA MPANGO WA MIKOPO YA MAJIKO YA UMEME NA VITUO VYA KUCHAJI MAGARI YA UMEME
Na Janeth Raphael MichuziTv Serikali imezindua rasmi mpango wa ukopeshaji wa majiko ya umeme kwa wateja wa TANESCO pamoja na mradi wa vituo vya kuchajia vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme, hatua inayolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi, kupunguza gharama za maisha kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya utekelezaji wa mpango huo iliyofanyika jijini Dodoma, Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi (Mb.), alisema miradi hiyo ni sehemu ya matokeo ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika sekta ya umeme na kwamba sasa wananchi wanaanza kunufaika moja kwa moja na maboresho hayo. Amesema matumizi ya umeme katika kupikia na usafiri yatawezesha familia nyingi za Kitanzania kupunguza matumizi ya fedha kwa ajili ya nishati, kuongeza muda wa kufanya shughuli za maendeleo na kuboresha mazingira ya maisha kutokana na matumizi ya nishati safi. Waziri Ndejembi ameeleza kuwa Serikali inaona matumizi ya umeme katika …