TANAPA, WADAU WA UTALII WASUKA MIKAKATI KABAMBE KUELEKEA MSIMU MPYA WA UTALII
TANAPA, WADAU WA UTALII WASUKA MIKAKATI KABAMBE KUELEKEA MSIMU MPYA WA UTALII
Na. Calvin Katera - Babati. Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imekutana na wadau wa utalii na uhifadhi ili kusuka mikakati itakayochagiza ongezeko la watalii na kuridhika kwa wageni watakaotembelea Hifadhi ya Taifa Tarangire. Mikakati hiyo imefanyika leo Juni 03, 2026 katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika hifadhi hiyo inayosifika kwa tembo wengi na wakubwa nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Kikao hicho ni hatua ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa utalii (High season) unaoanza mwezi Juni hadi mwishoni mwa mwezi Januari kila mwaka. Katika kikao hicho Mkuu wa Kanda ya Kaskazini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Dkt. Beatrice Kessy alieleza kuwa wadau na wawekezaji kwa kushirikiana na hifadhi wanapaswa kutoa huduma bora zitakazoongeza hamasa na kuridhika kwa wageni ili waende kuisemea vizuri hifadhi na Taifa kwa ujumla. Kama inavyojulikana katika soko la utalii mgeni anaporidhika kwa huduma na mapokezi mazuri anaporudi nchini kwake huwa ni balozi mzuri kwa ya…