TAKUKURU YAKABIDHI VIFAA TIBA KWA WATOTO WALIOZALIWA KABLA YA WAKATI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA
TAKUKURU YAKABIDHI VIFAA TIBA KWA WATOTO WALIOZALIWA KABLA YA WAKATI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila (kulia), akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila, vifaa tiba kwa ajili ya watoto njiti vilivyotolewa na watumishi wa TAKUKURU. Na Kadama Malunde – Shinyanga Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imekabidhi vifaa tiba vya kisasa kwa ajili ya kuwahudumia watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto. Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na mashine ya kutoa joto kwa watoto wachanga (Radiant Warmer) na mashine ya kutibu ugonjwa wa manjano kwa watoto wachanga (Phototherapy Machine) , ambavyo vimenunuliwa kupitia michango ya hiari ya watumishi wa TAKUKURU nchini. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Juni 3, 2026, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila, amemkabidhi vifaa hivyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa y…