SERIKALI YAZINDUA GRAND CHALLENGES TANZANIA KUCHOCHEA UBUNIFU WA KUTATUA CHANGAMOTO ZA TAIFA
SERIKALI YAZINDUA GRAND CHALLENGES TANZANIA KUCHOCHEA UBUNIFU WA KUTATUA CHANGAMOTO ZA TAIFA
SERIKALI imezindua jukwaa jipya la kitaifa la ubunifu litakalowawezesha wanasayansi, watafiti na wabunifu kubuni suluhisho za ndani kwa changamoto zinazoikabili nchi katika sekta za afya, usalama wa chakula, mabadiliko ya tabianchi na teknolojia, hatua inayotarajiwa kuharakisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Jukwaa hilo linalofahamika kama Grand Challenges Tanzania (GC-TZ) linalenga kuunganisha watafiti, watunga sera, sekta binafsi na washirika wa maendeleo ili kutumia sayansi, teknolojia na ubunifu katika kutatua changamoto za maendeleo na kuimarisha ustawi wa wananchi. Akizindua jukwaa hilo jijini Dodoma tarehe 04 Juni, 2026, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidhi Ameir, alisema mpango huo umeanzishwa wakati Tanzania inaanza kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga uchumi shindani, unaojitegemea na unaowajumuisha wananchi wote. Alisema pamoja na mafanikio yaliyopo, nchi in…