SERIKALI YATOA MSUKUMO MPYA WA NISHATI SAFI KWA KUPUNGUZA KODI ZA MAGARI YA UMEME NA GESI

SERIKALI YATOA MSUKUMO MPYA WA NISHATI SAFI KWA KUPUNGUZA KODI ZA MAGARI YA UMEME NA GESI
Na Janeth Raphael MichuziTv - Bungeni Dodoma Serikali imeendelea kuweka msukumo mkubwa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi na mbadala nchini, hususan umeme na gesi asilia, katika sekta ya usafiri na matumizi ya majumbani, kupitia mapendekezo mapya ya hatua za kodi kwa mwaka wa fedha 2026/27. Akiwasilisha mapendekezo ya Serikali ya makadirio ya mapato na matumizi Bungeni, Waziri wa Fedha,Balozi Dkt Khamis Mussa Omar, amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kifedha na kodi zinazolenga kupunguza gharama za uwekezaji na kuongeza matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira. Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, Serikali imeendelea kutoa msamaha wa ushuru wa bidhaa kwa magari yanayotumia umeme na gesi asilia kwa kuzingatia ukubwa wa injini, sambamba na msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) inayotumika kwenye magari. Aidha, Serikali imeondoa VAT kwenye vifaa vinavyotumika katika miundombinu ya gesi asilia (CNG), ikiwemo compres…