SERIKALI YASISITIZA NAFASI YA UTAFITI KATIKA KUJENGA UCHUMI WA MAARIFA
SERIKALI YASISITIZA NAFASI YA UTAFITI KATIKA KUJENGA UCHUMI WA MAARIFA
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM Serikali imesisitiza umuhimu wa kuimarisha elimu, utafiti na ubunifu kama nguzo muhimu za kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga uchumi wa kisasa unaotegemea maarifa, teknolojia na ushindani wa kimataifa. Msisitizo huo umetolewa leo Juni 11, 2026 na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu, alipomwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, katika hafla ya kufunga rasmi Maadhimisho ya Kumi na Moja ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Dkt. Nungu amesema mafanikio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 yatategemea kwa kiasi kikubwa uwezo wa mfumo wa elimu kuzalisha wataalamu wenye ujuzi wa kisasa, maadili mema, uwezo wa kubuni teknolojia na kutatua changamoto zinazolikabili taifa. Amesema Serikali inaendelea kuimarisha sekta ya elimu kupitia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2…