SERIKALI YAPONGEZA UJIO WA VYUO VIKUU BORA VYA MALAYSIA TANZANIA
SERIKALI YAPONGEZA UJIO WA VYUO VIKUU BORA VYA MALAYSIA TANZANIA
Na Mwandishi Wetu WAZAZI na wanafunzi nchini wamefurahishwa na maonesho ya vyuo vikuu Malaysia ambavyo vimewapa fursa mbalimbali za masomo nchini humo kwenye maonesho yaliyofanyika jana. Akizungumza kwenye maonesho hayo, Mratibu wa maonesho, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Elimu Vyuo Vikuu, Global Education Link, (GEL), Abdulmalik Mollel, alisema maonesho yametoa fursa nyingi kwa vijana. Alisema vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefika kwenye maonesho hayo na kwamba kama kuna waliokosa nafasi wafike Global Education Link ambako watapatiwa fursa kama hiyo ya kuvijua vyuo hivyo “GEL inawahimiza wanafunzi, wazazi na walezi waliokosa kuhudhuria Maonesho ya Study in Malaysia katika Hoteli ya Serena kufika ofisi za GEL, ambako huduma za ushauri, udahili, scholarship na mwongozo wa kusoma Malaysia zinaendelea kutolewa kama ilivyokuwa kwenye maonesho,” alisema Mollel. Mollel alisema maonesho hayo ya Study in Malaysia yamefungua fursa za Scholarship kwa wanafunzi wa Tanzania na kuonge…