SERIKALI YAOMBA AWAMU YA PILI YA MRADI WA MAZIWA FAIDA KUANZA MWAKA 2027

SERIKALI YAOMBA AWAMU YA PILI YA MRADI WA MAZIWA FAIDA KUANZA MWAKA 2027
Na Hadija Bagasha  -  Tanga Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeomba kuendelea kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland kupitia utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Maziwa Faida kuanzia mwaka 2027 hadi 2032, ili kuendeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kuimarisha uzalishaji wa maziwa, kuongeza tija na kuboresha maisha ya wafugaji nchini. Ombi hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Fabian Madele, wakati akifungua rasmi Maonesho ya Ubunifu na Teknolojia katika Sekta ya Maziwa (TALIRI Open Day 2026) yaliyofanyika katika Kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kanda ya Mashariki, jijini Tanga. Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Madele amesema Mradi wa Maziwa Faida unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania kupitia TALIRI na Taasisi ya Maendeleo ya Kilimo na Chakula ya Ireland (TEAGASC), kwa ufadhili wa Serikali ya Ireland kupitia Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania, umeleta mageuzi makubwa katika se…