SERIKALI YAHIMIZA WAZAZI/WALEZI MALEZI YA WATOTO

SERIKALI YAHIMIZA WAZAZI/WALEZI MALEZI YA WATOTO
Na Jackline Minja, Dodoma Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, amewahimiza wazazi na walezi kuimarisha malezi ya watoto wao na kutoa taarifa mapema kwa maafisa ustawi wa jamii pale wanapobaini changamoto zinazoweza kuhatarisha ustawi wa mtoto. Mhe. Mahundi ametoa wito huo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Martha Festo Mariki leo Juni 19, 2026 bungeni Dodoma, ambapo amebainisha kuwa Serikali imeendelea kuimarisha mikakati mbalimbali ya kukabiliana na tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani nchini, ikiwemo kutoa elimu kwa wazazi na walezi, kuimarisha uchumi wa kaya na kuboresha huduma za ustawi wa jamii. Amesema Serikali imeweka mkazo katika kuelimisha wazazi na walezi kuhusu wajibu wao wa kuwalea na kuwatunza watoto ili kuwazuia kukimbilia maisha ya mitaani. "Serikali inaendelea kutoa elimu kwa walimu na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola mara mtoto anapopot…