SERIKALI YAHAKIKISHA MAZINGIRA BORA KWA SHULE BINAFSI
SERIKALI YAHAKIKISHA MAZINGIRA BORA KWA SHULE BINAFSI
SERIKALI imezitaka taasisi binafsi za elimu kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa mageuzi ya elimu yanayolenga kuimarisha ujuzi, sayansi na teknolojia, huku ikiipongeza Shule ya Kimataifa ya Luminous kwa mchango wake katika kukuza ubora wa elimu nchini. Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid J. Maulid, alipomwakilisha Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, katika Mahafali ya Pili ya Shule ya Kimataifa ya Luminous yaliyofanyika Juni 14, 2026 jijini Dar es Salaam. Dkt. Maulid alisema Serikali imeendelea kufanya maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo pamoja na mitaala ili kuhakikisha mfumo wa elimu unazalisha wahitimu wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira na maendeleo ya teknolojia. Aidha, alibainisha kuwa Serikali inajiandaa kukabiliana na ongezeko kubwa la wanafunzi watakaojiunga na elimu ya sekondari ifikapo mwaka 2028, hali inayotarajiwa kuongeza mahitaji ya miundombinu na rasilima…