SERIKALI YAFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI KUPITIA MRADI WA UMEME MBANDE- KONGWA

SERIKALI YAFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI KUPITIA MRADI WA UMEME MBANDE- KONGWA
Na Dotto Kwilasa, Dodoma Kukamilika kwa mradi wa kimkakati wa Kituo cha Kubadilishia Njia za Usambazaji Umeme (Switching Station) na Transforma ya Kudhibiti Umeme katika eneo la Mbande, Wilaya ya Kongwa, kunatajwa kufungua ukurasa mpya wa uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi katika ukanda wa kati wa Tanzania. Mradi huo uliotekelezwa na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 10.5, unalenga kuongeza uhakika wa huduma ya umeme na kuweka mazingira bora kwa ukuaji wa shughuli za uzalishaji mali. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo Juni 16, 2026, Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema upatikanaji wa umeme wa uhakika ni nguzo muhimu ya maendeleo ya viwanda, biashara, kilimo cha kisasa na utoaji wa huduma za kijamii. Amesema mradi huo utaimarisha usambazaji wa umeme katika Wilaya za Kongwa, Gairo, Chamwino na baadhi ya maeneo ya Mpwapwa, hatua itakayochochea uwekezaji na kuongeza tija katika shughuli mbalimbali za kiuchumi. “Se…