SERIKALI YAFAFANUA JINSI WANAWAKE WA VIJIJINI WANAVYONUFAIKA NA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YA HALMASHAURI

SERIKALI YAFAFANUA JINSI WANAWAKE WA VIJIJINI WANAVYONUFAIKA NA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YA HALMASHAURI
SERIKALI YAFAFANUA JINSI WANAWAKE WA VIJIJINI WANAVYONUFAIKA NA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YA HALMASHAURI Na Janeth Raphael MichuziTv Bungeni - Dodoma  Serikali imeeleza kuwa imeweka mifumo na taratibu mbalimbali za kuhakikisha wanawake wa vijijini wanapata fursa sawa ya kunufaika na mikopo inayotolewa kupitia asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri nchini. Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Dkt Festo Ndugange wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Dkt. Neema Peter Majule, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuhakikisha fedha hizo zinawafikia wanawake wa vijijini. DKt Ndugange amesema kuwa kwa sasa utoaji wa mikopo hiyo unafanyika kupitia mfumo wa kielektroniki wa WEZESHA Portal, ambao umeboreshwa ili kutoa nafasi kwa makundi maalumu, ikiwemo wanawake wa vijijini, kuwasilisha maombi yao kwa urahisi na kwa wakati. Amesema pamoja na matumizi ya mfumo huo wa kidijitali, Serikali imewaelekeza Watendaji wa Kata na Vijiji kuwasaidia wananchi…