SERIKALI YAENDELEA KUWAWEZESHA VIJANA, WASHIRIKI 100 BORA WACHAGULIWA VIJANA UCHUMI CHALLENGE 2026
SERIKALI YAENDELEA KUWAWEZESHA VIJANA, WASHIRIKI 100 BORA WACHAGULIWA VIJANA UCHUMI CHALLENGE 2026
Na Dotto Kwilasa,Dodoma Katika kuendeleza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita za kukuza ubunifu na kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya uchumi wa Taifa, washiriki 100 bora wamechaguliwa kuendelea na hatua inayofuata ya Shindano la Vijana Uchumi Challenge 2026 baada ya ushindani mkubwa ulioshirikisha maombi 7,852 kutoka mikoa yote ya Tanzania. Akizungumza jijini Dodoma June 4,2026 Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya Vijana Uchumi Challenge, Amina Sanga, amesema shindano hilo lenye kaulimbiu “Wanafikiri, Taifa Linasonga” limebeba dhamira ya kuibua mawazo bunifu ya vijana yatakayochangia kuimarisha uchumi wa Tanzania, kukabiliana na athari za misukosuko ya kiuchumi duniani na kuunga mkono utekelezaji wa maono ya Serikali ya Awamu ya Sita pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Amesema mwitikio wa vijana umekuwa wa kuvutia, ambapo sekta ya TEHAMA na huduma za kidigitali imeongoza kwa asilimia 30.7 ya mawazo yaliyowasilishwa, ikifuatiwa na kilimo na teknolojia za kilimo…