SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA WATUMISHI WA UMMA KUPITIA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI
SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA WATUMISHI WA UMMA KUPITIA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI
Na Antonia Mbwambo- Mbeya Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa Watumishi wa Umma kupitia utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute, wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba za watumishi katika Shule za Msingi Ngolela, Wilaya ya Kyela na Idweli, Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya, iliyohusisha wataalamu kutoka Ofisi hiyo pamoja na Watumishi Housing Investments (WHI). Bw. Allute amesema makazi bora yataongeza ari ya kazi kwa Walimu na kuboresha utoaji wa huduma. Aidha, amewataka Watumishi watakaonufaika na nyumba hizo kuzitunza vizuri mara zitakapokamilika kwa kuwa ni mali za umma na zinazopaswa kudumu ili kuwanufaisha Watumishi wa baadae. "Serikali inaendelea kuwekeza fedha nyingi katika kuboresha mazingira ya kazi kwa Wa…