SERIKALI KUENDELEA UBORESHA NA KUJENGA MIUNDOMBINU YA UVUVI
SERIKALI KUENDELEA UBORESHA NA KUJENGA MIUNDOMBINU YA UVUVI
NA MWANDISHI WETU – SONGEA Serikali inaendelea kuboresha na kujenga Miundombinu ya uvuvi ikiwemo masoko ,maghala ya kuhifadhia mazao ya uvuvi, vichanja vya kukaushia samaki maghala ya kuhifadhia mazao ya uvuvi na viwanda vya kuchakata mazao ya uvuvi na teknolojia rafiki za ukaushaji ili kubadilisha sekta hiyo kutoka ufugaji na ukulima mdogo kuelekea katika kuimarisha lishe na uchumi wa wakulima wadogo wanaojikita katika uzalishaji na ukuzaji wa viumbe maji nchini ambapo matokeo hayo yanatarajia kuchochea uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla. Hayo yameelezwa na Bw. Jumanne Mwankoo Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma wakati wa tukio la kuhakiki taarifa ya matokeo ya mwisho ya mradi wa kuimarisha lishe kwa wakuzaji wadogo wa viumbe maji (ARNSA) uliokuwa ukiratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Uratibu wenye Ulemavu kwa msaada wa Shirika la NORAD kupitia Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo Duniani IFAD tarehe 5 Juni 2026.Bw. Mwankoo alisema kuwa Mradi huo wa kikanda uliokuwa …