SANGU :MAHUSIANO MEMA NI MSINGI WA KUIMARISHA UMOJA NA DEMOKRASIA NCHINI
SANGU :MAHUSIANO MEMA NI MSINGI WA KUIMARISHA UMOJA NA DEMOKRASIA NCHINI
Na. OWM (KAM), Morogoro Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Deus Sangu amesema mahusiano mema, mazungumzo ya kujenga na mshikamano wa kitaifa ni nguzo muhimu katika kuimarisha demokrasia, amani na maendeleo endelevu nchini. Akifungua Warsha ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Juni 17, 2026, mjini Morogoro, Waziri Sangu alisema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote wa kisiasa kwa kuzingatia misingi ya kuheshimiana, ushirikishwaji na kutanguliza maslahi ya Taifa. Alisema viongozi wa vyama vya siasa wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha mazungumzo yenye kujenga, kudumisha amani na kuimarisha mshikamano wa kitaifa badala ya kuhimiza migogoro. “Mahusiano mema ndiyo msingi wa amani, umoja na maendeleo ya Taifa. Tunaposhirikiana kwa heshima na maelewano bila kujali tofauti zetu za kiitikadi, tunajenga Taifa imara lenye mshikamano,” alisema Waziri Sangu. Aidha, aliwataka viongozi hao kushirikiana na Serikali katika ut…