SAMIA ATANGAZA UTALII ALIPANIA SOKO LA URUSI

SAMIA ATANGAZA UTALII ALIPANIA SOKO LA URUSI
Na Beda Msimbe,TBN, Petersburg, Urusi Ushirikiano wa miaka 65 ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Urusi sasa unatafsiriwa kuwa daraja imara la maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku sekta ya utalii ikichukua mwelekeo mpya wa kimkakati kuvutia masoko ya kimataifa likiwemo la Urusi. Alisema anatambua soko la Urusi ni kubwa naTanzania ipo tayari kulihudumia kwa kuondoa vikwazo kadhaa ikiwamo kuwezesha kupatikana kwa safari za moja kwa moja kutoka Moscow hadi Dar es Salaam na Zanzibar. Rais alisema hayo wakati akihutubia wawakilishi kutoka nchi 130 duniani zilizoshiriki mkutano wa kiuchumi wa kimkataifa wa Petersburg Juni 5, 2026. Katika jukwaa hilo la kiuchumi, Rais Samia alitangaza kuwa kuanzia Julai 2 mwaka huu, Shirika la Ndege la Tanzania, Air Tanzania, litaanza safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam, Moscow, na Zanzibar kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii hadi kufikia laki tano ifikapo mwaka 2030 na hatimaye milioni moja. Hatua hii inaenda sambamba na ushindi wa tuzo za kimatai…