RIDHIWANI: UTUMISHI WA UMMA UENDANE NA KASI YA TEKNOLOJIA
RIDHIWANI: UTUMISHI WA UMMA UENDANE NA KASI YA TEKNOLOJIA
Ahimiza matumizi AI kurahisisha utoaji huduma za umma Na. Jawadu Kinyobwa – Dar es salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb), amesema utumishi wa umma unapaswa kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa pande zote za Muungano. Mhe. Kikwete amesema hayo Junin17, 2026 katika Kongamano la Pili la Utumishi wa Umma Tanzania 2026 lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNCC) jijini Dar es Salaam, ambalo limewakutanisha wadau mbalimbali kujadili nafasi ya utumishi wa umma katika kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050. Amesema utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 unahitaji utumishi wa umma wenye uwajibikaji, ufanisi, ubunifu na uwezo wa kusimamia kwa mafanikio sera na mipango ya Serikali ili kutoa huduma bora kwa wananchi na kujenga imani kwa Serikali yao. “Dira ya Taifa …