RC CHALAMILA AFANYA KIKAO KAZI NA WENYEVITI, WATENDAJI WA KATA NA MITAA DSM
RC CHALAMILA AFANYA KIKAO KAZI NA WENYEVITI, WATENDAJI WA KATA NA MITAA DSM
-Atoa maagizo lukuki ya kuboresha Mkoa huo kuelekea AFCON 2027. -Ataka muonekano mzuri wa Jiji kwa kufanya usafi wa mazingira na kuondoa kabisa gereji bubu barabarani. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wamiliki wa gereji na mafundi seremala kuondoa vyuma chakavu na samani chakavu maeneo ya barabarani ili jiji liwe nadhifu huku akiwataka Madiwani, wenyeviti wa mitaa,watendaji wa kata na mitaa pamoja na wakuu wa wilaya zote tano kushiriki kikamilifu katika ulinzi na usalama wa maeneo yao na Mkoa huo kwa ujumla ikiwemo kuanzisha vikundi vya sungusungu Akizungumza katika katika kikao kazi maalum kilichokutanisha Madiwani, wenyeviti wa mitaa,watendaji wa Kata na Mitaa pamoja na wakuu wa wilaya zote tano za Mkoa huo Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila amesema vyuma hivyo chakavu kwenye maeneo ya barabara vimekuwa vikiharibu muonekano wa jiji huku pia akisisitiza serikali mkoani humo haitokuwa tayari kuona amani ya mkoa huo inavurugwa kwa kuwa mkoa huo …