RAISSA TRAVELS TANZANIA YAJIVUNIA KUPANUA WIGO WA HUDUMA ZA SAFARI NDANI NA NJE YA NCHI
Mtendaji wa safari na utalii,Lucia Mbwambo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampuni hiyo jijini Arusha ……….. Na Happy Lazaro, Arusha Katika kipindi ambacho mahitaji ya huduma za safari na utalii yanaendelea kuongezeka, Kampuni ya RAISSA TRAVELS TANZANIA imeendelea kujiimarisha kwa kupanua huduma zake na kuwafikia wateja wa makundi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Mtendaji wa Safari na Utalii wa kampuni hiyo, Lucia Mbwambo, amesema kampuni hiyo imeendelea kujenga rekodi nzuri ya utoaji wa huduma za kitaalamu jambo ambalo limeifanya kuaminiwa na wadau wengi wa sekta ya usafiri, utalii na biashara. Amesema kampuni hiyo imewekeza katika utoaji wa huduma jumuishi za usafiri ikiwemo ukataji wa tiketi za ndege za ndani na kimataifa, uratibu wa safari za ndani na za Kimataifa, huduma za maombi ya viza, uwekaji wa nafasi za malazi katika hoteli mbalimbali, bima za safari pamoja na usaidizi wa pasipoti na nyaraka nyingine muhimu za usaf…