Rais wa Singapore awasili nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu

Rais wa Singapore awasili nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu
Rais wa Jamhuri ya  Singapore Mhe.Tharman Shanmugaratnam, amewasili nchini  kwa Ziara ya Kitaifa ya siku tatu, Juni 8-10, 2026. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Mheshimiwa Tharman Shanmugaratnam akiwa ameambatana na Mwenza wake Mama Jane Ittogi, alilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo(Mb) ambaye aliambatana na viongozi wengine waandamizi wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila  na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania, Mhandisi Peter Ulanga. Ziara ya Kitaifa ya Rais Tharman Shanmugaratnam, ni ya kwanza kufanywa na Rais wa Singapore tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia 1980. Ziara hii inaashiria hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia, biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Singapore. Akiwa nchini Mheshimiwa Rais Tharman atapokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mheshimiwa Dkt. Sam…