RAIS WA NAMIBIA AWASILI KWA ZIARA YA KITAIFA NCHINI TANZANIA
RAIS WA NAMIBIA AWASILI KWA ZIARA YA KITAIFA NCHINI TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, amewasili nchini kwa Ziara ya Kitaifa ya siku tatu kuanzia tarehe 19 hadi 21 Juni 2026, kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Nandi-Ndaitwah alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Serikali. Katika mapokezi hayo pia alikuwepo Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini Tanzania, Mhe. Gabriel Sinimbo. Ziara hiyo inafanyika katika kipindi ambacho Tanzania na Namibia zinaendelea kuimarisha uhusiano wao wa kihistoria uliojengwa katika misingi ya mshikamano wa harakati za ukombozi wa Afrika, urafiki wa muda mrefu na ushirikiano wa karibu katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Akiwa nchini, Mhe. Rais Nandi-Ndaitwah anatarajiwa kufanya mazungumzo ya uwili na mwenyeji wake…