RAIS DKT. SAMIA KUPOKEA GAWIO LA SERIKALI JUNI 30 IKULU DAR ES SALAAM
RAIS DKT. SAMIA KUPOKEA GAWIO LA SERIKALI JUNI 30 IKULU DAR ES SALAAM Naibu Msajili wa Hazina, Lightness Mauki, amesema Serikali itaendelea kuimarisha uwazi, uwajibikaji na usimamizi wa uwekezaji wa umma ili kuhakikisha rasilimali zilizowekezwa katika taasisi, mashirika ya umma na kampuni zenye hisa za Serikali zinaendelea kuleta tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Bi. Mauki amesema hayo leo Juni 15, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, Morocco Square jijini Dar es Salaam, ambapo alitangaza rasmi kufanyika kwa Siku ya Gawio 2026 itakayofanyika Juni 30, 2026 katika Ikulu ya Dar es Salaam. Alisema mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambaye atapokea gawio na michango mbalimbali kutoka taasisi za umma pamoja na kampuni ambazo Serikali imewekeza. “Tunawashukuru sana waandishi wa habari kwa kuendelea kuitikia mwito wetu na kuonesha thamani yenu kama wadau muhimu wa uwajibikaji na uwazi katika usimamizi wa uwekezaji wa Serikali. Kupitia k…